01/06/2020
Wandugu, kwa miaka mitatu sasa nimekuwa na safari za kwenda Mahak**ani ambapo nilikuwa na kesi, gazeti lilichukua habari yangu wakaigeuza yao na kuiuza bila ruksa yangu wala kunitambua kwenye maandishi kuwa mimi ndiyo chanzo cha habari hiyo...Sasa kwenye uandishi wa habari hilo ni kosa...
Tabia hii ya waandishi wa habari / wahariri wanaojidhania "wana majina makubwa" mimi nimekuwa mhanga kwa muda mrefu, toka miaka ya 1990s,
Nikaamua kuacha kuandikia magazeti ya Tz..
Mtandao ulipokuwa nikawa naandika kwa nadra mtandaoni...
uandishi wangu ni wa kifalsafa zaidi, na kiuchunguzi, na kiurasini - mantiki, siyo siasa, itikadi wala dini k**a ilivyozoeleka Tz.
Lakini hata huko jamaa wakachukua habari yangu na kuigeuza yao...
Nilipowauliza kunani? hawakunijibu, jeuri ya ulimbukeni, ya kuyakuta maisha ya middle class ukubwani..!
Nikawauliza tena wandugu vipi..? Wala hawakutaka kuniona...dhalau kwani nitawafanya nini? Who is Nsajigwa? Si ni jamaa tu wa mtaani..?
Sasa nikawa na option mbili, aidha "nimuachie Mungu" k**a ilivyozoeleka au nijipiganie mwenyewe kwa akili zangu, potelea mbali matokeo yoyote, kwa kuwa mimi ni freethinker kwa falsafa ya maisha yangu, suala la "kumuachia mungu" halipo...
Ikabidi tu niwapeleke mahak**ani, nikajisimamia mwenyewe kesi bila wakili, nikisaidiwa na kaka mdogo (sasa ndugu yangu) mwanafunzi tu wa sheria (wao waliweka wakili, ni gharama sana kuweka wakili, yabidi umlipe kila anapokwenda mahak**ani, kwa kesi inayoendelea muda mrefu unaweza ishia njiani ukafilisika kwa madeni)...
Hayo hapo chini ni matokeo ya kesi hiyo, dharau ni mbaya, ulimbukeni ni tatizo...wangekubali tu tuonane wakakubali kosa lao tusingefikishana huko...
Matokeo ya kesi yalikuwa mei /14/2020 wiki mbili zimepita. Nilikuwa kimya mpaka rafiki yangu kijana mwingine mwandishi alipojua hili na kuniambia kaka litoke public, ili iwe fundisho kwa jamii...
Kisheria jamaa wanaweza kukata rufaa, inaruhusiwa, na ikiwa hivyo kesi itahamia Mahak**a ya juu zaidi.
K**a nilivyokwisha amua, nitajipigania mimi mwenyewe mpaka akili yangu ya mwisho...siogopi kwenda Mahak**ani wala siogopi kulumbana kisheria na mawakili, mimi elimu falsafa, lojiki, urasini mantiki, kujiuliza maswali muda wote na kuutafuta na kuuonyesha ushaidi hivyo vyatosha, na hata sheria, nililazimika kusoma vitabu vyao ili kujua kanuni za msingi zinazoendesha kesi, hizi za civil, k**a vile ilivyo kwamba hata k**a hujawahi kucheza soka au mchezo wa bao au chess, unapouangalia utauelewa vizuri pale unapojua sheria na kanuni zake.
Hakika siku za mbeleni natia nia ya kuandika juu ya uzoefu wa kwenda Mahak**ani, nimeyakuta mengi huko...
Freethinker FearlessThinker Fikrahuru Nsajigwa Nsa'Sam MWASOKWA