09/04/2024
Mshahara hautoshi? Muda pia umekubana na unatamani kufanya biashara?
Ajira hufika kikomo, ni muhimu kuanza kufanya biashara ukiwa bodo kwenye ajira, kwanza itakupa uzoefu na kuijua biashara. Usisubiri ustaafu ukaja chagua biashara yoyote.
Shida ambayo wanapata waajiriwa hasa ni muda na kupata msimamizi sahihi wa biashara.
Sasa, Fanya biashara zifuatazo.
1. Jifunze kutengeneza bidhaa za kijasiriamali. Hapa unaweza kufanya biashara kwa kutengeneza bites kwa muda wako wa ziada na kupeleka madukani, pia unaweza tengeneza cakes, juice, sabuni za maji, tengeneza icecream nk. Vyote hivi unatengeneza kwa muda wako wa ziada.
2. Biashara ya mtandao(network marketing).
Hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa muda mchache kwa siku au kwa wiki na ukaanza kujitengenezea kipato ukiwa umeajiriwa. Kupitia biashara hii wewe unakuwa msambazaji wa huduma au bidhaa kwa njia ya kuwaambia wengine uzuri wa bidhaa au huduma zile na wanaponunua wewe unapata kamisheni. Wengi hukosea kwenye uchaguzi wa kampuni, ukipata kampuni sahihi zenye bidhaa nzuri hii ni biashara nzuri( naweza kukuelekeza namna ya kuifanya.)
3. Biashara ya furniture. Kwakua Muda wako unabana unaweza kuanzisha biashara ya furniture. Unaweza kuuza vitanda, meza, makabati, showcase, viti nk. Hii unauza bidhaa zinazohesabika hivyo unaweza kujua umeuza kiasi gani hata k**a haupo.
4. Uza huduma na bidhaa mtandaoni za Afya, Urembo,electronics nk. Tafuta chochote cha kuuza online unakua unapokea simu tu.
Anzisha Blog, weka mambo mbalimbali juu Passion yako(Mfano mahusiano, mahubiri, mapishi, michezo, siasa, udaku nk).
5. Fanya biashara za ufugaji. Wanyama, ndege na samaki.
I hope hii itakusaidia, follow page yetu ili uendelee kujifunza zaidi
SAVE POST hii itakusaidia siku za baadae