mahamudutwar

mahamudutwar welcome to get best and qwarit furniture

23/09/2024
20/08/2024

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa zinazosambaa kuhusu mwenendo wa tukio la kikatili lilitokea dhidi ya Binti mmoja Mkazi wa Dar es salaam ambalo lilirekodiwa katika video zilizosambaa zikionesha Binti huyo akifanyiwa vitendo vya ubakaji, kulawitiwa na kushurutishwa kuomba msamaha kwa ‘Afande’ ambapo pamoja na kusikitishwa, LHRC imesema inajiuliza maswali mengi kuhusu taarifa za Jeshi la Polisi tangu kuibuka kwa tukio hilo.

Taarifa iliyotolewa leo Aug 19,2024 na Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Anna Henga imenukuliwa ikiuliza maswali 11 yafuatayo…….

1. Taarifa zipi ni sahihi kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu, Wizara Mambo ya Ndani au Mak**anda wa Polisi wa Mikoa wa Dar es salaam na Dodoma?

2. Je Watuhumiwa ni Maafisa wa Jeshi lipi?

3. Watuhumiwa katika tukio hilo walikuwa watano, je huyo mwingine ni nani na yuko wapi?

4. Binti alilazimishwa kumuomba msamaha ‘Afande’, je Afande ni nani?

5. Je Muhanga yupo salama katika mikono ya wanaomhumkumu kuwa ni k**a alikuwa anajiuza?”

6. Je Binti huyo kuwa katika mikono ya Polisi hakutaathiri
upatikanaji wa haki na ushahidi?

7. Je Mtu kuwa k**a anajiuza inahalalisha kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwepo kubakwa?

8. Je kwa vitendo hivi Jeshi la Polisi linasimamia maslahi ya nani?”

9. Je kuwa Mlevi na mvuta bangi ni kinga dhidi ya uhalifu?

10. Kwa kutajwa Afande bila kusema ni Afande wa Jeshi gani je Polisi hawana mgogoro wa maslahi na hili shauri?

11.Taarifa ya Polisi ya August 9 2024 ilisema upelelezi umekamilika na leo ni tarehe 19, je ni lini shauri hili litapelekwa Mahak**ani?”

“LHRC inapenda kuwakumbusha kuwa kitendo alichofanyiwa Muhanga ni cha kinyama, kikatili, kinyume na haki za binadamu na sheria za Nchi na kwamba yeyote atakayefumbia macho vitendo hivyo ni adui wa haki na utu, LHRC inapenda kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kuacha kulinda na kutetea uhalifu kwani kauli ya RPC Dodoma ni wazi inatetea Wahalifu na Uhalifu uliofanyika, pia Polisi itoe nafasi kwa Binti Muhusika kupata huduma ikiwepo ya ushauri nasihi kutoka kwa Chombo ambacho hakina maslahi na shauri hili” ——— imeeleza taarifa ya LHRC.

10/11/2021

Address

Nyahanag
Kahama

Telephone

+255765488778

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when mahamudutwar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share