12/02/2026
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imepiga marufuku kutumia noti kutengeneza mashada ya maua na mapambo mengine, ikisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria, na ni uharibifu wa tunu ya taifa.
Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel Tutuba amesema watakaobainika kutenda kosa hilo wanaweza kukabiliwa na adhabu ya faini ya hadi shilingi milioni tano.